USHIRIKISHWAJI MADINI KUINUA UCHUMI TAIFA

:::::::::

Imeelezwa kuwa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya Madini nchini itasaidia kuendelea kukuza Uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka wizara ya Madini Augostine Ollal wakati akizungumza kwa niaba ya Naibu katibu Mkuu wiza ya madini katika zoezi la kufunga jukwaa la nne la ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya Madini lililokuwa likifanyika Jijini Mwanza

Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya madini Mhandisi Theonestina Mwasha ameelezea umuhimu wa jukwaa hilo ambapo pia amewasisitiza makampuni ya uchimbaji wasambazaji huduma Pamoja na watoa huduma kutekeleza matakwa ya kanuni za ushirikishwaji wa watanzania ili matokeo Chanya yaweze kuonekana 

Aidha Mkurugenzi wa ukaguzi wa biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki amezungumzia maazimio Matano ya jukwaa hilo











 

Related Posts