Mwanza. Rais Samia Suluhu Hassan amezinduliwa daraja la JPM maarufu kama Kigongo-Busisi leo Juni 19, 2025 mkoani Mwanza.
Daraja hilo la sita kwa urefu barani Afrika limejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh700 bilioni. Utekelezaji wa mradi huo ukifanywa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation na China Railway 15 Bureau Group Corporation.
Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3, upana wa mita 28.45 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 1.66 lilianzwa kujengwa Februari 25, 2020 na kukamilika 2025.
Daraja hilo pia lina njia mbili za magari zenye upana wa mita saba kila upande na njia za waenda kwa miguu kila upande yenye upana wa mita 2.5 na maegesho ya dharura yenye upana wa mita 2.5 kila upande. likipita juu ya maji ya Ziwa Victoria kuunganisha eneo la Kigongo, Wilaya ya Misungwi na Busisi, Wilaya ya Sengerema.