Makocha wapewa akili Taifa Cup

Katibu mkuu wa  chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Kigoma Anasi Kibonajoro ameishauri mikoa iwe  inatumia wachezaji wake katika mashindano ya Taifa Cup.

Kibonajoro aliyasema hayo kutokana na kasumba iliyokuwepo ya  viongozi wa mkoa, kutegemea wachezaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema hata kama ni wazawa wa mkoa fulani, kuwatumia wachezaji wa mkoa husika kutaifanya mikoa iwe na maendeleo.

“Kwa kweli  kutegemea wachezaji wa Dar es Salaam, kunaweza kupoteza nafasi ya kuonekana wachezaji wanaotoka katika mikoa,” alisema Kibonajoro.

Wakati huohuo, baadhi ya makocha kutoka mikoa ya Mara na Pwani na wengine wakiwatumia waakilishi wao,  walionekana katika uwanja wa Donbosco Upanga   wakifuatilia Ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL).

Makocha hao, walikuwa na lengo la kutafuta wachezaji watakaochezea mikoa yao katika mashindano ya Taifa Cup.

Mashindano ya Taifa Cup yamepangwa kuanza Juni 24, katika uwanja wa Chinangali, Dodoma.

Related Posts