Opah Clement kurudi Ligi Kuu China

BEIJING Beikong inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake China iko kwenye mpango wa kumsajili nyota wa zamani wa Simba, Opah Clement.

Hivi karibuni, Opah aliachana na FC Juarez ya Mexico baada ya kuhudumu kikosini hapo msimu mmoja akitokea Henan Jianye ya China.

Chanzo kiliambia Mwanaspoti Beijing inataka kuweka ofa nzuri kumnasa mshambuliaji huyo kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano.

Kiliongeza Opah atasaini kikosini hapo kama atashawishiwa na ofa nzuri kwani pia ana ofa kutoka nchi nyingine.

“Beijing wanapambana ili kumpata Opah, walishawahi kuona kiwango chake alipokuwa anakipiga Henan ya nchini humo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

Msimu uliopita, Opah alicheza mechi sita kati ya 17 zilizochezwa na FC Juarez bila ya kufunga bao wala kutoa asisti.

Akiwa na Jianye ya China alifunga mabao matano na kumaliza msimu akiwa miongoni mwa 10 bora ya wafungaji, mbele ya Yuan Cong aliyeongoza kwa mabao tisa.

Ukiachana na Simba Queens msimu wa 2021/22 ambako alipata mafanikio makubwa ya soka la wanawake, nyota huyo alichezea Kayseri Kadın ya Uturuki kwa mkopo 2022, msimu uliofuata akasajiliwa Besiktas ya nchi hiyo na 2023/24 akiichezea Henan Jianye ya China kwa msimu mmoja.

Kwa jumla hadi sasa, Opah amefunga mabao 16 kwenye timu tatu alizopita tangu aondoke Simba Jianye na Kayseri Kadın alifunga mabao matano, huku Besiktas ya Uturuki akiweka kambani mabao sita.

Related Posts