Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Queen Fraison almaarufu kama Bonge la Dada, kwa sasa ni moto wa kuotea mbali! Sio kwa sababu ya kiki tu, bali miondoko yake ya mauno, tabasamu lake la kuvutia na muonekano wake wa kipekee vimewafanya wanaume wengi kupoteza dira, huku wake zao wakibaki na maswali.
Wake wa watu wanadaiwa kuanza kuonyesha wasiwasi kuhusu tabia za waume zao kuchelewa kulala au kuwa busy na simu kumbe wanachungulia maonyesho ya Queen Fraison bila hofu!
Jamani, kila ukifungua simu anakimbilia kuangalia huyu Bonge la Dada! Eti anacheza tu, anaburudika! Nimechoka! alisikika mwanamke mmoja akilalamika kwenye kundi moja la WhatsApp la kina mama.
Taarifa zinasema kuwa baadhi ya familia ziko kwenye hali tete baada ya wanawake kugundua kuwa wapenzi wao wamekuwa mashabiki wa karibu sana wa Queen huyo.