WAKUNGA SASA KUJIFUNZA POPOTE KUPITIA SIMU – TEKNOLOJIA YAZINDULIWA

::::::

Na Mwandishi Wetu – Dar es salaam

SERIKALI kwa kushirikiana na Ubalozi wa Denmark nchini wamezindua rasmi programu maalumu itayotumiwa na wakunga kujifunza namna ya kutoa huduma bora na kuongeza weledi katika huduma inayoitwa ‘Safe delivery App’.

Programu hiyo imezinduliwa kupitia mradi wa “10 milioni safe birth initiative” utakaotekelezwa katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2027.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Ziada Sellah amesema mradi huo umekuja wakati sahihi kwasababu mkunga anaweza kujifunza mahali popote pale akiwa kazi, nyumbani hata kama hamna mtandao akishapakua anafungua kawaida.

“Akipata changamoto anaweza kuona nini cha kufanya kupitia hiyo na kama application iliyozinduliwa leo tuna magroup ya WhatsApp na inawezekana mkunga yuko Rufiji akapata changamoto anaeleza kwenye hayo magroup ili wapate msaada.

PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY
 

Related Posts