…………
Na Ester Maile Dodoma
Bilioni tatu zitatumika katika ujenzi wa sekondari ya wavulana bunge katika kata ya kikombo mkoani Dodoma kilomita moja kutoka shule ya sekondari ya wasichana bunge.
Ameyabainisha hayo leo 26 June 2025 jijini Dodoma Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson wakati akizindua ujenzi huo kata ya kikombo.
Dkt Tulia amewashukuru wadau waliojitoa kwa hali na mali katka kufanikisha zoezi la kuchangi ujenzi huo pia amepongeza Taasisi za kifedha na wabunge kwa kuchangia kupitia kwenye posho zao ilikufanikisha ujenzi huo.
Hata hivyo Dkt Tulia ametoa waito kwa wadau ambao hawajachangia kuweza kuchangia hata mtu mojamoja unaweza kuchangia na kwa wale walio ahidi vifaa vya ujenzi wanatakiwa kupeleka ili ujenzi uwezekuanza mara moja.