Kama hujui Tausi Royals imewekwa mtu kati na timu tatu zinazoifuatia katika msimamo wa Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanawake (WBDL) ikiwa inashiriki kwa mara ya pili na mara hii hadi sasa inaongoza katika msimamo ikiwa na pointi 14. Timu zingine zenye pointi 14 ni Jeshi Stars, JKT Stars na DB Troncatti.
Kasi ya Tausi Royals imezishtua timu zingine zinazoifuatia, huku zikionekana kutoa sapoti kwa timu zinazocheza nayo.
Baadhi ya michezo ambayo Tausi Royals imebakiwa nayo ni dhidi ya Jeshi Stars, JKT, Stars, DB Troncatti, Reel Dream, Ukonga Queens, DB Trocantti, Vijana Queens na DB Lioness.