CCM Yatangaza Idadi ya Wagombea Ubunge, Zaidi ya 4,000 Wajitokeza – Video – Global Publishers



Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa jumla ya wanachama 4,109 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo yote 272 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, ambaye alieleza kuwa kati ya waliochukua fomu hizo:

3,585 ni kutoka Tanzania Bara,

524 ni kutoka Zanzibar.

Makalla alisema zoezi hilo linaonesha hamasa kubwa ya kisiasa ndani ya chama, huku akisisitiza kuwa CCM itaendelea kufuata misingi ya haki, usawa na demokrasia katika mchakato mzima wa kupata wagombea wake rasmi.

“Hii inaonesha ni kwa kiasi gani wanachama wetu wamekuwa na imani kubwa na chama, na wako tayari kulihudumia taifa kupitia CCM,” alisema Makalla.

Kwa sasa, hatua inayofuata ni mchujo ndani ya chama ambapo wagombea watakaopitishwa wataingia kwenye kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.











Related Posts