Beki Che Malone Kukutana na “Thank You” Simba – Global Publishers



Beki wa kazi ndani ya kikosi cha Simba, Che Malone

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Simba, Che Malone mambo ni magumu katika kikosi hicho akitajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watakutana na Thank You kuelekea 2025/26.

Tayari Fabrince Ngoma ni uhakika hatakuwa ndani ya Simba SC msimu ujao baada ya mkataba wake kugota mwisho. Che Malone jina lake linatajwa kuwa miongoni mwa watakaopewa Thank You pia ndani ya kikosi hicho ambacho hakijatwaa taji loloye msimu wa 2024/25.

Ni mabao mawili alifunga beki huyo msimu uliopita akicheza jumla ya mechi 25 za Ligi Kuu Tanzania Bara NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.











Related Posts