*Aweka mikakati ya kuinua vijana katika mafunzo ya ufundi stadi
Mamlaka ya Elimu Mafunzo ya Ufundi (VETA) imesema kuwa kuna mageuzi katika utoaji wa mafunzo ya ufundi yanayochochea katika kuandaa nguvu kazi katika viwanda pamoja kuongeza fursa za ajira kwa vijana za kujiajiri au kuajiriwa.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakati alipotembelea Banda la VETA kwenye maonesho ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
CPA Kasore amesema kuwa katika mageuzi ya VETA ni kuleta fani zinazoendana na mahitaji yaliyopo katika mazingira yanayozunguka jamii katika kutatua changamoto zinazotokana na kukosekana kwa mafunzo ya ujuzi na ufundi Stadi.
Aidha amesema katika ufundishaji wa wanafunzi ni tofauti kwani anaanza kulijua soko akiwa katika mafunzo na anapohitimu anaingia moja kwa moja katika ajira au kujiajiri.
Amesema kuwa kuna wahitimu wa vyuo ambao wamepata ujuzi ambao wameanza kuzalisha bidhaa na kuingiza katika soko kwa kupata wanunuzi.
Aidha amesema kuwa wajasiriamali wanaongia kwenye mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali wanaongeza thamani ya bidhaa hizo na kupata tija ya kuongeza kipato.
CPA Kasore amesema Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan vyuo 80 vimejengwa na vyuo 65 viko katika hatua za ujenzi awali ambapo vyuo hivyo vitakuwa 145 nchi nzima.
Amesema kuwa katika Sekta ya kilimo wamekuja na bunifu ya mashine ya kupukuchulia mahindi na sekta mifugo wamekuja na mashine ya kutengeneza vyakula vya kuku pamoja na mashine ya kutotoleshea vifaranga.
Hata hivyo amesema VETA imeanzisha kampuni Tanzu ambapo bunifu hizo zitapatikana kwa kuuzwa lengo ikiwa ni kuendeleza bunifu hizo kwa kufanya kazi na sio kuzifungia.
Amesema tofauti ya maonesho hayo VETA imekuja na vitu ambavyo wanaweza kujifunza watoto katika kuwaandaa mapema katika ujuzi.
Amesema Sera ya Elimu iliyozinduliwa inatoa majibu ya namna ya kufanya mafunzo ya ufundi Stadi yanakwenda kuchochea uchumi kwa vijana wa kitanzania.
Mkurugenzi wa VETA CPA Anthony Kasore akiwa katika picha mbalimbali za kutembeleea Banda la VETA ,Sabasaba jijini Dar es Salaam.