Waziri Ajiua Kwa Risasi Kisa Kufutwa Kazi Na Putin – Global Publishers



Vladimirovich Starovoit, aliyekuwa Waziri wa Usafirishaji wa Urusi kati ya mwaka 2024 na 2025

Vladimirovich Starovoit, aliyekuwa Waziri wa Usafirishaji wa Urusi kati ya mwaka 2024 na 2025, amekutwa amefariki dunia kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kujiua kwa kujipiga risasi, muda mfupi baada ya Rais Vladimir Putin kumfuta kazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya usalama vya Urusi, mwili wa Starovoit, mwenye umri wa miaka 53, ulipatikana ndani ya gari lake katika eneo la viunga vya Moscow mapema Jumatatu asubuhi. Tume ya Uchunguzi ya Shirikisho (Investigative Committee) imethibitisha tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya kifo hicho.

Rais wa Urusi, Vladimir Vladimirovich Putin

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Starovoit huenda alikumbwa na mshtuko mkubwa wa kisaikolojia baada ya kutangaziwa kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, hatua ambayo ilitangazwa rasmi na Kremlin kupitia amri ya rais iliyotolewa Jumapili usiku.

Roman Starovoit alizaliwa Januari 20, 1972, na alijizolea umaarufu kama mtaalamu wa miundombinu na usafirishaji nchini Urusi. Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Usafirishaji mnamo mwaka 2024, alihudumu kama Gavana wa Kursk Oblast kwa muda wa miaka kadhaa. Pia alikuwa mkuu wa Rosavtodor, shirika la shirikisho linalosimamia miundombinu ya barabara.


Related Posts