Wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali zinazotelewa hapa katika Viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa “SabaSaba”Ukitembelea Banda la UDOM utapata huduma ya afya bure, msaada wa kisheria bure, kujua miradi inayotekelezwa UDOM, tafiti mbalimbali, watoto kujifunza Uchoraji na huduma nyinginezo.
Watumishi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwahudumia wananchi mbalimbali waliotembea banda la chuo hicho katika katika viwanja vya Saba Saba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,MMG )