Na Mwandishi wetu
SERIKALI imewatoa hofu Watanzania kuhusu hoja ya kuwa utekelezaji Dira 2050 unaweza kukumbwa na changamoto ya uhalali wa kisheria na hivyo mpango huo muhimu kwa taifa ukawa na ombwe la kiufanisi hapo baadae
Akiongea katika kikao maalum na Wahariri kutoka jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaii Profesa Kitila Mkumbo amesema Dira ya taifa 2050 imewekewa ulinzi kwa kupelekwa bungeni na kwamba hakuna Rais atakayeweza kwenda kinyume na uamuzi huo
Profesa Mkumbo amesema Dira 2050 itatekelezwa na Marais watatu,na kwa atakaetaka kuibadilisha atatakiwa kupeleka bungeni na kwamba Dira hii imekuwa tofauti kwa kuwa ya 2025 iliishia hatua ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri tu.
Waziri huyo amesema mchakato wa kutengeneza Dira 2050 umepitia hatua 13 ambazo ni kuandaa na kuidhinisha miongozo ya Dira.
Mkakati wa kuandika Dira ulianza Aprili mwaka 2023, kwa kuunda vyombo vya kutathimini mchakato wa Dira,kufanya tathimini ya utekelezaji wa Dira 2025.
Pia kukusanya maoni ya wananchi na wadau juu ya maudhui gani yaingie kwenye Dira,kujifunza kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Marekani kwa hatua zilizopigwa.
Alizitaja baadhi ya nchi walizojifunza ni Botswana, Moroco,Mauritius, Afrika Kusini na Kenya.
Kwa Asia wamejifunza Kusini mwa Asia za China,Indonesia,Korea Kusini,Singapore na India,na kwamba kwa Ulaya wamejifunza kidogo kutokana na kwamba historia yao si ya muda mrefu kama nchi zenye historia 1,000.
Hatua nyingine ni uchambuzi,uandishi na uhariri wa tqarifa na kutoa Rasimu ya kwanza ya Dira 2050.Pia kulinda rasmu ya kwanza ya Dira 2050 ilizinduliwa Desemba 2024,na kuchukua Rasimu kupeleka tena jwa wadau ili kupata maoni ya kihariri.
“Tulikutana na wadau mbalimbali kama waandishi wa habari na vyama vya siasa ili kupata makubaliano ya pamoja.Tulivyokutana na vyama vya siasa tulikubaliana tusibishane juu ya tunakwenda wapi ila tukubaliane tuende huku,Ilani zetu ziakisi tunaenda wapi,”amesema.
Hatua nyingine, kutoa rasimu ya pili ya Dira ya Taifa na kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu,Juni 2025 iliidhinishwa na Baraza la Mawaziri na kufuatiwa na Bunge.
Aidha,amesema hatua ya mwisho ni kuutaarifu umma kuwa mchakato wa Dira umekamilika na itajulikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza Dira 2050 Tanzania Tuotakayo,na hatua ya mwisho ni Rais Samia Suluhu Hassan kuizundua Julai 17,mwaka huu.