Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania, Rose Alphonce Nungu almaarufu kama Muna Love, ametoa ujumbe mzito wa hamasa unaogusa maisha ya kila mmoja hasa katika nyakati ambazo watu wengi hupitia changamoto za mahusiano na maisha ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake, Muna ameandika:
“Usiruhusu mtu anayejaribu kupoteza furaha yako awe karibu nawe kwenye maisha yako. Itakusaidia kufocus na kufanya vikubwa. Akija tena anakuta nafasi imejaa, na hatojaribu tena.”
Ujumbe huu umeonekana kuwagusa mashabiki wake wengi ambao wameonyesha kuungana naye kwa namna ya kipekee kupitia maoni na kushare ujumbe huo.
Muna Love ni miongoni mwa wasanii waliowahi kupitia misukosuko mikubwa ya maisha lakini ameendelea kusimama imara na kuwa mfano wa mwanamke anayepambana, akiibuka mara kadhaa na kuonyesha nguvu ya mwanamke jasiri katika jamii ya Kitanzania.