TUME YA MADINI YANG’ARA SABASABA KUPITIA HUDUMA BORA ZA MAABARA

-Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere, Dar es Salaam

Meneja wa Huduma za Maabara wa Tume ya Madini, Mhandisi Mvunilwa Mwarabu, ameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na maabara ya Tume katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba (DITF).

Huduma hizo ni pamoja na uchambuzi wa sampuli za madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya XRF, utoaji wa ushauri wa kitaalam kwa wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na wawekezaji, pamoja na kusaidia kuhakikisha usahihi wa taarifa za kijiolojia na ubora wa madini yanayochimbwa nchini.

Wananchi wengi wameonyesha kuvutiwa na huduma hizo huku wakiahidi kuzitumia kwa maendeleo ya shughuli zao za madini.




Related Posts