Israel Yadaiwa Kujaribu Kumlipua Rais Mpya wa Iran – Global Publishers



(Kushoto) Waziri Mkuu Wa Israel, Benjamin Netanyahu ; (Kulia)Rais wa Iran Masoud Pezeshkian

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ametoa madai mazito kwamba Israel ilijaribu kumuua wakati wa mvutano mkubwa wa kijeshi kati ya mataifa hayo mwezi uliopita. Akizungumza katika mahojiano ya dakika 28 yaliyofanyika na mtangazaji wa kihafidhina wa Marekani, Tucker Carlson, Pezeshkian alisema kwamba alilengwa moja kwa moja na jeshi la Israel, lakini shambulio hilo lilishindwa kufanikiwa.

Pezeshkian alisema kuwa shambulio hilo lilifanyika katika eneo alilokuwapo kwa ajili ya kikao cha siri, ambapo Israel ilipata taarifa kupitia wapelelezi wake na kujaribu kulipua eneo hilo. Hakutaja tarehe ya tukio hilo wala kama lilitokea wakati wa vita vikubwa vya mwezi Juni kati ya Iran na Israel. “Kwa hakika, si Marekani iliyokuwa nyuma ya jaribio hilo… ilikuwa ni Israel,” alisema Pezeshkian kupitia tafsiri ya kutoka Kifarsi kwenda Kiingereza.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran yaliibuka baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuweka muda wa mwisho wa siku 60 kwa Iran kukubali makubaliano mapya ya nyuklia. Israel ilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi ambayo ililenga viongozi wakuu wa jeshi la Iran, wanasayansi wa nyuklia, na maeneo ya kurutubisha uranium. Mashambulizi hayo yalifanyika katika vituo vya Natanz, Fordo, na Isfahan.


Related Posts