Charles Barnabas Kiongozi wa Ubia na Uhusiani wa Mradi wa masuala ya Nishati wa Services Modern Energy Cooking ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAD) kupitia ubalozi wa Uingereza Tanzania aki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo tar 10 July 2025.
Mwakilishi wa Kampuni inayojishughulisha na matumizi ya nishati safi majiko ya kutumia umeme SESCOM Shabani Selemani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo tar 10 July 2025
NA MUSSA KHALID
Watanzania wametakiwa kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa badala yake watumie nishati safi ili kuendana na adhma ya serikali ya awamu ya sita ya mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kaili hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Charles Barnabas Kiongozi wa Ubia na Uhusiani wa Mradi wa masuala ya Nishati wa Services Modern Energy Cooking ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAD) kupitia ubalozi wa Uingereza Tanzania wakati wakifanya mradi wa Pikasmati katika eneo la Mwenge.
Amesema kuwa wanafanya kampeni ya mradi wa Pikasmati lengo lake ni kuongeza uelewa kwa wananchi kutumia matumizi ya nishati safi kwa kupika kwa umeme ili kuendana na dhamira ya serikali ya matumizi ya nishati safi.
“Tunawapa elimu wananchi watambue kwamba kupika kwa umeme sio gharama kubwa kwani kuna majiko ambayo ni fanisi kwa ajili ya matumizi hayo na elimu hii ndio imekuwa ikifanya watu waweze kutambua matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia’amesema Charles
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni inayojishughulisha na matumizi ya nishati safi majiko ya kutumia umeme SESCOM Shabani Selemani amesema matumizi yake yanasaidia kuonda gharama na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Nao baadhi ya wananchi Anamery George kutoka Kigamboni Twangoma na Oliver John Mkazi wa Ubungo wameelezea umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia katika utunzaji wa mazingira lakini pia inatunza muda sambamba na kuokoa gharama.
Imeelezwa kuwa Kampeni hiyo ya Pikasmati ni ya Kitaifa ambayo inajumuisha maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Zanzibar ambapo itafanyika mpaka mwezi wa 12 mwaka huu ili watanzania wafahamu kuwa kupikia kwa umeme ni nafuu.