Vodacom na Stanbic wakabidhi msaada wa miche na vifaa mkoani Singida

*Ni kupitia Msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama

Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania, Chiha Nchimbi (kulia) na Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Geofrey Mwijage (kushoto), wakikabidhi miche 100 ya miti kwa Mkuu wa Divisheni ya Awali na Msingi wa Manispaa ya Singida, Omari Maje, katika Shule ya Msingi Minga mkoani Singida. Ikiwa ni sehemu ya msafara unaoendelea wa Twende Butiama ulioanza Julai 3 mwaka huu, msafara huo pia ulikabidhi magodoro 30, vitanda vitano, mashuka 20, madawati 10 na vitimwendo 6 (wheelchairs) kwa shule hiyo. Shughuli hizi zinafanyika kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania na Benki ya Stanbic Tanzania.

 

Related Posts