RITA yaungwa mkono na Waziri Ndumbaro kwa huduma za vyeti Sabasaba.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewapongeza Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kuendelea kutoa vyeti vya kuzaliwa na kuomba wananchi waendelee kujitokeza ili wapatiwe huduma katika Maonesho ya Sabasaba.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kutembelea banda la taasisi hiyo lililopo kwenye maonesho ya kimataifa ya kibiashara (Sabasaba) leo Julai 11, 2025 Jijini Dar es Salaam. 
Dkt. Ndumbaro ameiopongeza RITA kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kusajili na kutoa cheti cha kuzaliwa hapo hapo kwenye maonesho hayo na kuwaomba wananchi kuendelea kujisajili na kuomba cheti kwa njia ya mtandao (online) kwa kutumia  eRITA popote ulipo.
Wakala unaendelea kutoa huduma ya ndoa na talaka, kuandika na kuhifadhi Wosia pamoja na huduma ya kusajili na kutoa cheti cha kuzaliwa.

Related Posts