Washiriki wa Msafara wa Twende Butiama 2025 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha safari yao wilayani Butiama mkoa wa Mara eneo ambalo amezikwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Msafara huu umefadhiliwa na Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na benki ya Stanbic Tanzania, ulipita katika mikoa 11 baada ya kuanzia safari jijini Dar es Salaam Julai 3 2025 na kufanikiwa kupanda jumla ya miti 50,000, kutoa msaada wa vifaa kwa shule za msingi 13 na kugusa maisha ya wanafunzi 15,000 pamoja na wale wenye mahitaji maalum na kutoa vifaa 562 na matundu ya vyoo 30.