ZAIDI YA KAMPUNI 15 ZAANZA KUWEKEZA KATIKA KONGANI YA VIWANDA

……………..

Na Ester Maile Dodoma 

Eneo la Mgodi wa Dhahabu wa  Buzwagi Mkoani Shinyaga sasa umegeuzwa na kuwa Kongani ya Viwanda ambapo Kampuni zaidi ya 15 za Kimataifa zitaanza kuwekeza  katika Mgodi huo baada ya shuguli za uchimbaji Dhahabu kumalizika

Akizungumza na Waandishi wa habari leo 14 julai Jijini Dodoma, mkuu wa mkoa  wa Shinyanga  Mboni Mohamed Mhita  wakati akielezea mafanikia ya mkoa huo kwa kipindi cha miaka minne kuusiana na maendeleo katika sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Miundombinu, Viwanda na Biashara, kuwa Kongani hiyo itajihusisha na shuguli mbalimbali za viwanda pamoja na madini 

Mhita ameongeza kuwa uanzishwaji wa Viwanda vikubwa, vidogo na vya kati kumechochea uwepo wa ajira Elfu hamsini.

Aidha, Ameongeza kuwa Mkopo wa Kiasi cha shilingi Bilioni 8.56 kimetolewa kwa vikundi 1,124 vya wanawake ,vijana na wenye ulemavu wamenufaika sambamba na kunusuru kaya  Masikini.

Related Posts