Mrisho Mpoto, msanii wa sanaa za maonesho na kughani, kupitia akaunti yake ya Instagram ametoa taarifa za kufiwa na mkewe ambaye alikuwa akiugua.
Akizungumza na mwandishi wa Global TV, Mpoto amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu.
Ameongeza kwamba asubuhi ya leo, Julai 15, 2025 alizidiwa ambapo alikimbizwa hospitali alikofikwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu.
Mpoto amesema kuwa msiba upo nyumbani kwake, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, Julai 16, Yombo jijini Dar es Salaam.