ZRA sasa kuitumia DTB ukusanyaji mapato kidigitali Zanzibar

Unguja. Ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Serikali, Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGaz) wamesaini makubaliano na Benki ya Diamond Trust (DTB) kuanza kukusanya kodi hiyo kupitia mfumo wa kidigitali wa Zanmalipo.

Hatua hiyo imefikiwa leo Julai 16, 2025 hivyo benki hiyo inakuwa miongoni mwa taasisi za fedha na ambazo zinakusanya kodi hiyo kwa ajili ya Serikali kupitia njia za kielektroniki.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Serikali Mtandao (eGaz), Dk Said Seif Said amesema ni jambo muhimu kwani ukusanyaji wa mapato ya Serikali ndio njia kuu ya kuleta maendeleo katika nchi hivy katika ushirkiano huo ni rashi

Amesema Zanzibar katika masuala ya digital haijakaa nyuma itaendelea kuhamasishaji mabadiliko ambayo yanaonekana kwa nchi nyingine basi yafikiwe Zanzibar.

“DTB wametuahidi kwamba wanaouwezo mkubwa katika masuala ya kidigitali na kifedha na kwamba tutashirikiana pamoja kuhakikisha kwamba Zanzibar inaweza kufanya mambo mengi ya kidigitali katika kuleta maslahi makubwa ya Zanzibar,” amesema.

Amesema Serikali haina upendeleo na inamualika kila mmoja katika kushirikiana kuleta maendeleo ya Zanzibar ili ipige hatua zaidi na kufikia malengo iliyojipangia kwa kuleta mabadiliko kwa wananchi.

Meneja wa Uwajibikaji wa Walipa kodi ZRA, Saada Kassim Khamis amesema kikawaida wanatumia benki tofauti katika ukusanyaji wa mapato, hivyo ni faraja katika mamlaka hiyo kuongeza wigo wa benki wanazotumia katika ukusanyaji wa mapato hayo.

“Pamoja na ushIrikiano kupitia Zanmalipo zote zinaongeza faraja katika ukusanyaji wa mapato maana tumeondoka kwenye fedha taslimu na sasa tunakusanya kupitia mifumo ya benki hivyo inasaidia kusogeza huduma kwa wananchi na serikali inafanya matumizi yake,” amesema Saada.

Amewasihi wafanyabiashara wazitumie taasisi hizo kulipa kodi kwa kutumia mifumo hiyo hata waliopo nje ya Zanzibar, kwani ni taasisi ambazo zimeaminiwa na Serikali kusaidia ukusanyaji wa kodi.

“ZRA na Egaz ni taasisi za Serikali ambazo zinashirikiana kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kwa asilimia 100 kwahiyo katika jitihada hizo tuwashukuru wenzetu wa DTB kwa kuja na mbinu za kuwa sehemu ya ukusanyaji wa mapato ya kodi,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTB, Ravneert Chowdhury amesema mfumo wa Zanmalipo ni daraja kati ya Serikali na wananchi na kwamba kuwa na mifumo inarahisisha utoaji wa huduma, kupunguza gharama na kuepusha muda kopotea katika upatikanaji wa huduma.

Amesema Benki hiyo ina mifumo imara kwa hiyo watahakikisha wanakuanya kodi ya Serikali ili itemize malengo yake ya kutoa huduma kwa wananchi.

“Kwa sasa aina mbalimbali za kodi na tozo zinaweza kulipwa moja kwa moja kupitia matawi ya DTB na kupitia huduma ya benki kwa njia ya mtandao,” amesema.

Malipo haya yanajumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT), Kodi ya miundombinu, ushuru wa bidhaa, kodi ya hoteli, kodi ya mighawa, kodi ya uendeshaji wa utalii, ada ya stempu, tozo ya huduma za uwanja wa ndege, tozo ya huduma za bandari, kodi ya mafuta, usajili wa magari, ada za leseni za udereva, pamoja na tozo ya usalama wa viwanja vya ndege,

Amesema benki hiyo imejipanga kutoa huduma kwa mashirika ya kibiashara pamoja na walipa kodi binafsi kwa kutoa suluhisho za malipo za haraka, salama na za kuaminika.

“Hatua hii ni sehemu ya mkakati mpana wa DTB katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia mabadiliko ya kidigitali na ujumuishaji wa kifedha kwa kushrikiana na taasisi muhimu za Serikali