MSAJILI WA HAZINA ASHIRIKI UZINDUZI DIRA 2050

::::::::::

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, leo, Julai 17, 2025, ameshiriki uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).

Uzinduzi huo umefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki katika utekelezaji wa Dira hiyo ili kufikia lengo kuu la kujenga Taifa jumuishi, lenye ustawi, la haki na linalojitegemea.