Mafunzo ya wanadhimu wa kijeshi kufungwa rasmi leo Tanzania

Dar es Salaam. Mafunzo ya ukufunzi wa Maofisa Wanadhimu wa Umoja wa Mataifa yamefungwa rasmi leo Julai 17, 2025 katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliolenga kuwajenga uwezo wakufunzi wa maofisa wanadhimu wa Umoja Mataifa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weldi.

Mafumzo hayo yalioanza kutolewa tangu Julai 7, yakihusisha nchi za Ghana, Nigeria, Vietnam, Botswana, Zambia, Tanzania huku wakufunzi wa mafunzo hayo wakitoka Tanzania, Brazil, Bangladesh, Nigeria na Marekani.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Meja Jenarali Amri Mwami, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema kuwa mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo wa kipekee maofisa wanadhimu, ili watakaporejea katika nchi zao, waweze kuwa wakufunzi bora wa masuala ya ulinzi wa amani.


“Mafunzo haya ni sehemu ya maboresho ya miongozo mbalimbali ambayo Umoja wa Mataifa umeyatoa na sisi hatuna budi kuwapa wanadhimu ili wawe walimu watakapokwenda kwenye nchi zao wawe walimu kwa wengine ili kuimarisha juhudi za dunia katika kudumisha amani,” amesema Mwami.

Aliongeza kuwa anatarajia kuwa mafunzo haya yataongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya ulinzi wa amani, na hivyo kusaidia kudumisha amani salama na yenye ufanisi zaidi.

Zoezi hilo pia liliudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns, ambaye alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya amani.

“Mafunzo haya yanasaidia katika kujenga mifumo ya ulinzi wa amani ambayo ni thabiti, yenye weledi na inayohitaji ushirikiano wa kimataifa,” amesema Emilly.

Mratibu wa Mafunzo hayo kutola Umoja wa Mataifa, Colonel Abdulwahab, amesisitiza kuwa washiriki wa mafunzo hayo wamepata maarifa mapya ambayo yatawawezesha kutoa mafunzo bora kwa maofisa wenzao.

“Mafunzo haya yamefanikiwa katika kuleta mabadiliko chanya katika uwezo wa maofisa hawa kutekeleza majukumu yao ya amani,” amesema Abdulwahab.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania, Brigedia Jenerali Mwita Itang’are, alitoa shukrani kwa washiriki wote na kusema kuwa hatua hii ni muhimu katika kudumisha amani duniani.


“Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa dunia inaendelea kuwa salama na yenye amani,” amesema Itang’are.

“Mafunzo haya ni mchango mkubwa katika kujenga jamii ya kimataifa inayozingatia amani na usalama,”

Kwa pamoja wakitarajia mafunzo hayo yaleta mabadiliko makubwa katika ulinzi wa amani duniani, wakisisitiza

Umuhimi wa juhudi za pamoja za kimataifa katika suala hilo.