MARA YAWEKA HISTORIA SEKTA YA MADINI

::::::::::

Na Ester Maile Dodoma 

Katika sekta ya madini, Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini ikiwemo dhahabu, fedha, shaba, chuma, madini ya ujenzi, madini ya viwandani na madini ya vito. Madini ya dhahabu ndio yanayochimbwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na madini mengine. 

Hayo yamebainishwa leo 18 julai 2025 jijini Dodoma na mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evansi Alfred Mtambi wakati akielezea mafanikio ya mkoa huo kwa kipindi vha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu Hassan

Mtambi amesema hadi kufikia Juni, 2025 Mkoa ulikuwa na lesseni 2,288 ambazo zinahusisha uchimbaji wa madini, utafiti, uchenjuaji na biashara ya madini.  

Hata hivyo Mkoa wa Mara umezalisha dhahabu yenye uzito wa tani 58.90 ikiwa na thamani ya shilingi trilioni 6.90 kutoka kwa wachimbaji wakubwa, wakati na wadogo. Aidha, katika kipindi hicho Serikali imekusanya maduhuli ya shilingi bilioni 568 kutokana na malipo ya mrahaba, ada ya ukaguzi kwenye mauzo ya madini, ada za leseni na tozo mbalimbali za vibali, ushuru wa huduma katika Halmashauri na kodi ya zuio inayokatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Vile vile Katika Sekta ya Madini kuna urudishwaji wa faida kwa jamii kutoka kwa wamiliki wa leseni na kampuni za uchimbaji madini (CSR). Kwa miaka hii minne kumekuwa na utekelezaji wa miradi 398 ya huduma za jamii yenye thamani ya shilingi bilioni 33.81 zitokanazo na CSR ya sekta ya madini.