Nyota wa zamani wa Klabu ya Young Africans (Yanga SC), Fiston Mayele, amebadili dini kutoka Ukristo na sasa ni Muislamu, ambapo atatumia jina jipya la kiislamu “Mahmoud”.
Mayele kwa sasa anakipiga katika klabu ya Pyramids FC ya Ligi Kuu nchini Misri, ambako ameendelea kuonyesha makali yake tangu ajiunge akitokea Yanga SC.
Uamuzi wake wa kubadili dini umepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wake barani Afrika, hasa kutoka Jangwani ambako alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu.
Hadi sasa, Mayele (sasa Mahmoud) bado hajazungumza kwa kina kuhusu sababu za mabadiliko hayo, lakini tayari ameshaanza kutambulika kwa jina lake jipya ndani ya Pyramids FC na miongoni mwa mashabiki wake.