ALIYEKUWA Kocha wa utimamu wa mwili wa Yanga Princess, Alli Mbaga ameaga rasmi kwenye kikosi hicho baada ya mkataba wake kumalizika na inaelezwa viongozi wa timu wameanza mazungumzo na Mzimbabwe Brenda Chaoor.
Brenda, ambaye aliwahi kuzifundisha Simba Queens kabla ya kutimkia Fountain Gate Princess ambako alihudumu kwa msimu mmoja.
Sasa inaelezwa kuwa anatajwa Jangwani na huenda akachukua nafasi ya Mbaga aliyeitumikia Yanga kwa takribani misimu miwili mfululizo.
Yanga wanamtazama Brenda kama mbadala wa kocha huyo kutokana na uzoefu alioupata wa kufundisha timu za Tanzania, na mambo yakienda sawa, huenda akaandika historia ya kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuzifundisha timu za watani.
“Ni kocha mzuri. Katika majina ya wale makocha wanaoangaliwa na Yanga, mmojawao ni yeye. Ukaribu wake na wachezaji ndani umewavutia zaidi. Nafikiri kama mambo yatakuwa sawa, ataondokea huko na yupo hapa Dar muda kidogo,” kilisema chanzo hicho.