RUGAMBWA ATEULIWA KAMATI YA MASHINDANO CHAMA CHA SOKA MKOA WA SONGWE

 


Chama cha Soka Mkoa wa Songwe imemtetua Ndugu Juvenalius Rugambwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Chama cha Soka Mkoani humo SOREFA. 

Rugambwa, ambaye mwezi wa Sita mwaka huu alichukua fomu ya kugombea nafasi ya kamati tendaji ya shirikisho la soka Tanzania TFF na kua ndo kijana mwenye umri mdogo kutia nia katika nafasi huku akienguliwa katika hatua ya usahili na kushindwa kufika hatua ya mwisho katika uchaguzi wa TFF ambao unatarajiwa kufanyika mwezi agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa Barua iliochapishwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Songwe Ndg Pius Francis, ya tarehe 17 Julai 2025 yenye kumbukumbu namba SOREFA/009,2025 Uteuzi huu umetokana na Mchango wa Rugambwa katika Maendeleo ya soka ndani na nje ya Mkoa wa Songwe. 

Rugambwa mwenye shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma na hivi sasa anachukua Shahada ya Umahiri (Masters) ya Usimamizi wa Miradi anafahamika kwa mapenzi yake makubwa ya soka huku akiwa ameshashiriki miradi mingi ya kukuza vipaji vya soka haswa ngazi ya vijana  na wanawake. 

Kupitia uteuzi huu atakuwa miongoni mwa wahusika wa kusimamia mashindano ya soka katika mkoa huo kuhakikisha mkoa wa Songwe unakua na soka la ushindani, na kuinua hadhi ya mashindano mbalimbali ya soka mkoani humo.

 Uwepo wake katika kamati ya mashindano SOREFA  unaongeza maarifa ya kitaaluma, weledi na utendaji katika kupambania maendeleo ya soka mkoa wa Songwe.