Mourice Sichone asalia Zambia | Mwanaspoti

KIUNGO mshambuliaji wa Trident FC, Mourice Sichone amesema ataendelea kusalia kikosini hapo kumalizia mkataba wake wa miezi minane iliyobaki.

Katika nusu msimu aliocheza, kinda huyo (17), ukiwa ni wa kwanza kwake kukitumikia kikosi hicho, alicheza mechi 18, akifunga mabao sita na kutoa asisti nane.

Akizungumza na Mwanaspoti, alisema alipata ofa kutoka timu mojawapo ya Ligi Kuu Zambia lakini ameshindwa kuondoka kutokana na pesa kubwa iliyowekwa na klabu yake ya kuvunja mkataba na ilitaka Sh30 milioni ili waweze kumuachia.

“Kiasi kilichowekwa ni kikubwa, nimeshindwa kuondoka. Nilikuwa na ofa nyingi hapa Tanzania, Afrika Kusini na Ulaya ambazo pia zilihitaji huduma yangu. Kwa hiyo, nimeamua kusalia tu nimalize muda uliobaki,” alisema na kuongeza:

“Timu haikutaka kuniachia kwa sababu washambuliaji kule mbele ni wachache, hivyo kwa sasa na-focus na timu ili niisaidie msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.”

Mbali na ofa hizo, kulikuwa na ofa ya kwenda Ulaya, limeishaje? “Ni kweli, kuna wakala mmoja alinitafuta wakati ule tulipokuwa kwenye mashindano ya WAFCON ya vijana. Nchi inaitwa Albania. Ile timu ilikuwa ya vijana U-19 ambao walikuwa wanacheza UEFA Champions League, lakini kulikuwa na changamoto, dili likakwama na siwezi kulielezea sana.”