::::::::
Na Ester Maile Dodoma
Mkoa wa Arusha umepokea shilingi bilioni 85.2 kwa ajili ya sekta ya kilimo na shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mifugo ambayo imetumika kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali.
Yamebainishwa hii leo 20Julai 2025 jijini Dodoma na Mkuu wa mkoa huo Kenani Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wahabari kuhusu mafanikio ya mkoa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Aidha Miundombinu ya umwagiliaji katika bonde la Eyasi imetekelezwa kwenye ukubwa wa eneo la Hekta 5,000 katika Kata za Mang’ola na Baray Wilaya ya Karatu kwa gharama ya shilingi bilioni 38.434. Mradi unatarajiwa kunufaisha wakulima 3,000 wa vitunguu na mazao mengine utakapo kamilika.
Hata hivyoUzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kufikia Tani 536,581 kutoka Tani 450,015 mwaka 2021 sawa na ongezeko la Tani 86,566 (19%).