MWANDISHI ASHINDA KWA KISHINDO UDIWANI VITI MAALUMU

……….

 Wanawake 10 Waibuka Washindi Viti Maalum vya Udiwani

Na mwandishi wetu, Morogoro 

MOROGORO.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umekamilisha zoezi la kihistoria la uchaguzi wa wawakilishi wa viti maalum vya udiwani katika wilaya zote nchini. Uchaguzi huu, uliofanyika jana, Julai 20, 2025 ni hatua muhimu ya kuimarisha ushiriki wa wanawake na makundi mengine katika siasa za ndani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na umefanikiwa kupata madiwani watakaoungana na wenzao kutoka kata mbalimbali.

Katika Wilaya ya Morogoro Mjini, ushindani ulikuwa mkali, huku jumla ya wagombea 31 waliteuliwa kuwania nafasi 10 za viti maalum. Madiwani hawa waliochaguliwa sasa wataungana na madiwani kutoka kata 29 za Manispaa ya Morogoro ili kuwakilisha maslahi ya wananchi na kusukuma gurudumu la maendeleo.

Katika matokeo ya kusisimua ya uchaguzi huu wa udiwani viti maalum Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Latifa Ganzel, mwandishi maarufu wa gazeti la Uhuru mkoani humo, ameibuka kidedea kwa kupata kura 934, akiongoza orodha ya washindi wengine.

Madiwani 10 walioongoza katika uchaguzi huu wa viti maalum Wilaya ya Morogoro Mjini ni

1.  Latifa Ganzel:934

2.  Batuli Kifea:794

3.  Grace Mkumbae:752

4.  Salma Mbandu:698

5. Imakulata Mhagama: 581

6.  Warda Bazia:562

7.  Rahma Maumba:560

8.  Magreth Ndewe:556

9.  Anna Kisimbo: 535

10. Amina Zihuye: 532

Viti maalum vya udiwani ndani ya CCM vinaendelea kuthibitisha umuhimu wake kama nyenzo muhimu ya kuimarisha ushiriki wa wanawake na makundi mengine katika siasa, huku vikiwa daraja la kuleta maendeleo chanya katika jamii na kuwafikia wananchi wa ngazi ya chini.