VIWANDA 1,542 VYAJENGWA GEITA

………,….

Na Ester Maile Dodoma 

Mkoa wa Geita umefanikiwa kujenga jumla ya viwanda 1,542 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu kutoka viwanda 824 vilivyokuwepo mwaka 2021 na kusaidia kuongeza ajira kutoka 927 hadi ajira 15,161 mwaka 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Ruben Shigella ameeleza hayo leo Julai 21, 2025 mkoani Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya mkoa huo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tunavyo viwanda vya kutosha, kwa kweli tunamshukuru Mheshimiwa Rais, viwanda vyetu vimeongezeka kutoka 824 mwaka 2021 mpaka 1,542 na hivyo kusaidia kuongezeka ajira kwa watumishi wetu kutoka 927 mwaka 2021 mpaka 15,161 mwaka 2025.” Alisema Shigella.

Hata hivyo Shigella amesema katika kipindi hicho pia mkoa umetoa jumla ya zleseni 1,469 za biashara kwa wafanyabiashara mkoani humo na kusaidia kuongeza pato la mkoa ambapo mpaka kufikia mwaka 2021 kulikuwa na leseni 1,346 tu .