Msaidizi wa Fadlu ajiondoa Simba

WAKATI Simba ikiendelea kutangaza orodha ya wachezaji watakaokuwa nje ya hesabu za timu hiyo kwa msimu ujao wakiwapa ‘Thank You’, kuna msaidizi mmoja wa kocha Fadlu Davids amejiondoa ghafla.

Aliyetangaza kujiondoa ni mtaalam wa takwimu za wachezaji, Culvin Mavunga aliyetangaza kuondoka ndani ya timu hiyo.

Mavunga aliyefanya kazi kwa miaka mitano Simba akitokea kwao Zimbabwe, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram saa chache zilizopita.

Katika ujumbe huo, Mavunga amewashukuru mashabiki wa Simba, Bodi ya Wakurugenzi, na benchi la ufundi likiongozwa na Fadlu kwa namna alivyofanya nao kazi kwa ushirikiano.

MSAID
MSAID

“Ukurasa wangu na Simba umefika mwisho, imekuwa misimu mitano ya kuvutia, tulishindwa, tukashindwa na kutoa sare,” ameandika Mavunga.

“Pongezi zangu za dhati ziwaendee mashabiki wa Simba, nyie ni watu wa muhimu, Bodi na uongozi wa Simba, ahsante kwa kila jambo.

“Benchi la ufundi la Simba, upendo sana na ninyi ni familia daima, wachezaji wa Simba nawapenda sana familia, kocha Fadlu ahsante kwa mafunzo.”