Aliyeua Wanafunzi Wanne Afungwa Kifungo cha Maisha – Global Publishers



Bryan Kohberger, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu katika sheria ya uhalifu, amehukumiwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa msamaha wa kifungo (parole) mnamo tarehe 23 Julai 2025 katika Mahakama ya Ada, iliyopo Boise, jimbo la Idaho.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya jopo la mahakama kuthibitisha kuwa Kohberger alihusika moja kwa moja katika mauaji ya kikatili ya wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Idaho Kaylee Goncalves, Madison Mogen, Xana Kernodle na Ethan Chapin yaliyotokea tarehe 13 Novemba 2022.

 

Mbali na kosa la mauaji, Kohberger pia alipatikana na hatia ya kosa la wizi lililotokea sambamba na tukio hilo.

Hukumu hii inafunga moja ya kesi iliyozua mjadala mkubwa nchini Marekani na kuvuta hisia kutoka kwa jamii ya wanafunzi na umma kwa ujumla.