AGNESS SULEIMAN ‘AGGY BABY’ ASHINDA TUZO MBILI AFRICA ARTS ENTERTAINMENT AWARDS 2025

 

Mrembo maarufu, mwenye vipaji lukuki na msanii mwenye ushawishi mkubwa katika jamii, Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby, ameweka historia mpya katika tasnia ya burudani na maendeleo ya jamii baada ya kutangazwa Mshindi wa tuzo mbili kubwa kwenye Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) 2025.

Tuzo hizo zilitolewa rasmi tarehe 25 Julai 2025 katika hoteli ya kifahari ya Protea Hotel Courtyard, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Aggy Baby ameshinda katika vipengele viwili vinavyothibitisha mchango wake mkubwa ndani na nje ya sanaa:

Best Inspirational Youth Icon / Motivator

Fastest Rising Foundation of Excellence (kupitia taasisi yake ya kijamii – Tupaze Sauti Foundation)

Ushindi huu si wa kawaida. Ni uthibitisho wa jitihada zake si tu kwenye muziki na burudani, bali pia kwenye kuhamasisha maendeleo ya vijana wa Kitanzania kupitia elimu, maadili na miradi ya kijamii.

Mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla wanahimizwa kuendelea kumuunga mkono msanii huyu wa kipekee, ambaye kwa sasa ni nembo ya ubunifu, kipaji na uzalendo wa kweli.

Aggy Baby si msanii tu – ni kielelezo cha matumaini, uthubutu na mabadiliko chanya kwa kizazi kipya.