Jerry Slaa, Zungu ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM kwa njia ya mtandao Ilala

Dar es Salaam. Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa CCM, Wilaya ya Ilala wameshatinga ukumbini tayari kusubiri mkutano huo  kuanza kwa njia ya mtandao.

Kati ya wajumbe waliofika ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Musa Azan Zungu, Waziri wa Mawasiliano, Habari na Tekbolojia, Jery Silaa,na Aden Rage aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba.

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Said Side, Katibu wa CCM wa Ilala, Chifu Sylevester Yeredi, Mbunge wa Viti Maalumu, Janeth Masaburi,  Katibu Mwenezi mkoa wa Dar es Salaam, Bananga Bananga, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mwenyekiti wa CCM Nyamagana, Peter Begga.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Katibu Mwenezi wa Wilaya, Mwinyimkuu Sangaraza, amesema maandalizi kwa upande wao yamekamilika ikiwemo ufungaji wa mtandao na runinga kwa ajili ya kufuatilia mkutano huo.

Sangaraza amesema katika mkutano huo pia wanatarajia kuwa na wajumbe wengine kutoka mkoani ambao wapo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli zao.

Kwa mujibu wa mwenezi huyo, wajumbe wa mkutano mkuu Ilala wapo 11.