Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wa kupanua demokrasia katika mchakato wa uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali umeongeza idadi ya wanachama wa CCM wanaoomba kugombea nafasi za uongozi.
Akizungumza leo Jumamosi, Julai 26, 2025, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliofanyika kwa njia ya mtandao, Samia amesema baadhi ya majimbo yamekuwa na wagombea kati ya 39 hadi 40.
“Mtakumbuka kwamba tulifanya maamuzi ya kutanua demokrasia katika kuchagua viongozi ngazi ya taifa lakini pia ngazi ya jimbo na kata. Jambo hilo limevutia wana-CCM wengi zaidi kuomba kugombea, kwa hiyo tumeona kwenda na watatu kati ya wagombea wote hao siyo jambo la busara. Lakini pia kamati kuu imebanwa na katiba, hatuwezi kuongeza majina bila ridhaa, hivyo tumeamua kuomba ruhusa ya kubadilisha katiba ili kuongezwa idadi ya wagombea kutoka watatu hadi wanne au watano kulingana na uhitaji,” amesema Samia.
Endelea kufuatilia Mwananchi