KIUNGO Mtanzania, Charles Mmombwa, Julai 31 na chama lake la Floriana FC watakuwa na kibarua kizito cha kupambania kuvuka raundi ya pili ya mashindano ya Europa Conference League dhidi ya Ballkani.
Floriana FC inashiriki Ligi Kuu ya Malta, maarufu kama Maltese Premier League, ambayo ni ligi ya daraja la juu katika mfumo wa soka nchini humo. Malta ni nchi ndogo ya visiwa iliyoko katika Bahari ya Mediterania kati ya Italia na Afrika Kaskazini.
Timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa barani Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Hii ni raundi ya pili ya kufuzu mashindano hayo na mechi ya kwanza Floriana ilipoteza kwa mabao 4-2 ugenini katika Uwanja wa MFA Centenary.
Mechi ya marudiano Floriana itakuwa nyumbani na ili ivuke raundi hiyo na kwenda raundi ya tatu, chama la Mtanzania huyo linapaswa kushinda kwa mabao 3-0 na isiruhusu bao.
Chama la Mmombwa lilianzia raundi ya kwanza na kupata ushindi wa jumla ya mabao 5-3 dhidi ya Haverfordwest.
Hata hivyo, Mtanzania huyo alicheza mechi zote tatu mbili za raundi ya kwanza na moja ya raundi ya pili kwa dakika zote 90 akifunga bao moja.