Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga wakati akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
Mtaalamu wa Usalama na Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao Yusuph Kileo akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojishughulisha na Masuala ya Teknonolojia ya KONCEPT GROUP Krantz Mwatepele akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Afya Intelligence Mr Harrison Mariki akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
Mkurugenzi wa Kampuni iinayojishughulisha na masuala ya usalama mtandaoni na uchumi kwa kidigitali ya Cerensic Afrika akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
…………………
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa mabadiliko ya Mapinduzi ya kidigitali yanayofanyika sasa yanalenga kuhakikisha kila mtanzania anaweza kupata faida na fursa za Akili unde.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga amebainisha hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizindua mkutano wa kwanza wa wa Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025) ambalo linafanyika kwa siku mbili Julai 28-29 mwaka huu likiiangazia nama ya utengenezaji fursa kwa vijana sambamba na kulinda maadili ya nchi.
Dkt Mwasaga amesema kuwa jukwaa hilo limeshirikisha Taasisi za Kitaifa na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Ujerumani,Ufaransa,Uingereza,Estonia pamoja na nchi za ukanda zinazokaribiana na Tanzania.
Aidha amesema kuwa licha ya watu kusema Akili Unde kuwa inaathari pia inafursa nyingi ikiwemo usalama wa jinsi ya kumlinda mlaji na mambo yote ya faragha na huduma za mawasiliano kuwafikia watanzania wote.
‘Ukingalia kauli mbiu ya jukwaa hili inasema kuangalisha kesho ya Tanzania ambayo itakuwa inatumia Akili Unde ambayo ni jumuishi na yenye maadili na kuangalia masuala yote yanayohusiana na taarifa ili kuleta maendeleo jumuishi ya kiuchumi na kijamii’amesema Dkt Nkunde
Mkutano huu umeleta pamoja wataalamu wa teknolojia, watunga sera, wawakilishi wa sekta binafsi, na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujadili mwelekeo wa AI nchini Tanzania. Aidha, mkutano unalenga kuweka msingi wa sera jumuishi na endelevu zitakazoiwezesha Tanzania kuongoza katika matumizi salama na jumuishi ya teknolojia ya Akili Bandia barani Afrika.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Usalama na Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao Yusuph Kileo amehamasisha namna ya kukabiliana na taarifa ghushi mtandaoni ambazo zimechagizwa na AI kuwa ni lazima taarifa sahihi kutoka kwenye chanzo na kwa wakati sahihi zinapatikana.
Baadhi ya wataalamu waliochirikia katika jukwaa hili akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojishughulisha na Masuala ya Teknonolojia ya KONCEPT GROUP Krantz Mwatepele pamoja na Ester mengi Mkurugenzi wa Kampuni iinayojishughulisha na masuala ya usalama mtandaoni na uchumi kwa kidigitali ya Cerensic Afrika wamepongeza jukwaa hilo kwa wataalamu kwani inasaidia taifa kutengeneza dira inayoendana na mabadiliko.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga kwa niaba ya serikali ya Tanzania amesaini Mkataba wa makubaliano wa mashirikiano na Serikali ya Urusi kupitia Andrey Maslov kutoka Taasisi ya HSE Center for African Studies.
Amesema Makubaliano hayo ni pamoja na kushirikiana kwa pamoja,kufanya program za maendeleo kwa pamoja katika masuala ya kitaalamu lakini pia kufanya kwa pamoja makongamano na matukio yanayohusiana na teknolojia nchini Tanzania na Urusi.
Pia amesema kupitia mkataba huo watabadilishana mambo ya kitaalamu na Wizara na wakuu wa wizara mbalimbali za urusi na nchini zikiwemo taasisi mbalimbali,lakini watakaa kwa pamoja na kungezeana ujuzi katika mafunzo ya wataalamu wanaomaliza vyuoni kwenda Urusi na wao kuja nchini.