Waliopenya ubunge majimbo Dodoma hawa hapa, yumo Ndugai

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimewateua watiania watano kwenda katika hatua ya mchujo wa kura za maoni katika Jimbo la Bahi mkoani Dodoma, ambao ni Keneth Moro, Robert Kamunya, Suphian Masasi, Mathias Olyamunda na Flora Kilangwa.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Julai 29, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla mbele ya waandishi wa habari, jijini Dodoma.

Kwa upande wa Kongwa, watiania 10 wameteuliwa ambao ni Job Ndugai, Emmanuel Mbena, Nyaya Mazanda, Deus Seif, Philip Chiwanga, Pascal Mahinyila, Dk Simon Ngatunga, Samora Mchanga, Isaya Moses na Elias Mdau.

Chamwino wameteuliwa sita ambao ni Deogratius Ndejembi, Hololeti Mgema, Rehema Kayombo, Vincent Chomola, Andrew Mwaluko na Joel Mwakanyaga.

Makalla amesema watiania saba wameteuliwa Mvumi ambao ni Livingstone Lusinde, Dk Michael Nsendekwa, Happyness Mgongo, Steven Ulaya, Nyemo Masimba, Nick Masanyaji na Amos Nsanjila.

Endelea kufuatilia Mwananchi.