Dar es Salaam. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewataja walioteuliwa kuingia kwenye mbio za kura za maoni za ubunge katika Mkoa wa Arusha uliofanywa na Kamati Kuu.
Arusha Mjini ni, Ally Babu, Hussen Gonga, Haminata Taule, Mustapha Nasoro, Paul Makonda, Rwembo Mgweno na Jaspha Kishumbua.
Jimbo la Arumeru Magharibi wameteuliwa wagombea sita, Dk Johanes Lukumai, Noha Mollel, Noel Emmanuel, Estar Mollel, Herietha Temu na Luten Kanali Medin.
Jimbo la Karatu, walioteuliwa wako watano, Cesilia Pareso, Daniel Telemay, Pantaleo Pareso, Patric Matei na Shedrack Kana. Wakati jimbo la Longido wameteuliwa wanne, akiwemo Steven Kiluswa, Petro Ngalikoni, Niclas Sengeu na Matha Ntoipo.
“Jimbo la Arumeru Mashariki walioteuliwa ni wako nane, Joshua Nasari, John Pallangyo, Johnson Sarakikya, Elisa Mbise, Profesa Daniel Pallangyo, Rose Urio, Wiliam Sarakikya na Angella Pallangyo,” amesema
Jimbo la Monduli, Makalla ametaja walioteuliwa wapo wagombea sita, Fredrick Lowassa, Wilson Kurambe, Isack Joseph, Nuru Adam, Biliuda Kisaka. Jimbo la Ngorongoro walioteuliwa wako sita, Profesa Kokel Melumbo, Elizabeth Gibaseya, Yanic Ndoiyo, Max Kamaoni, Rose Njiro, Silvanus Pinda.