Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina ya walioteuliwa kwenda kura za maoni kupitia majimbo ya Kagera huku Innocent Bashungwa akiwa miongoni mwa waliopendekezwa kupitia jimbo la Karagwe.
Bashungwa atachuana na wengine watano ambao ni Princepilus Rwazo, Adolf Rwantungamo, Devotha Alexander, Comfort Blandes na Akida Mnyambo.
Kwa mujibu wa Makalla jimbo la Biharamulo Magharibi walioteuliwa ni sita ambao ni Ezra Chilewesa, Benidict Kipeja, Oscar Mukasa, Antony Choya, Dk Magnus Bainyikila na Saada Kalabaki.
“Bukoba mjini wapo watano ambao ni Almasoud Kalumuna, Alex Muganyizi, Jamilla Emir, Johnson Mutabindwa na Kokufatuka Ruta. Bukoba Vijijini wapo wagombea sita ambao ni Jahson Rwekiza, Astid Peter, Faris Burhan, Edmund Rutaraka, Fahami Juma, Philbert Bagenda,” amesema Makalla.
Jimbo la Kwera walioteuliwa ni sita ambao ni Khalid Nsekela, Speransa Marko, Innocent Balikwate, Markson Bartazary, Steven Katemba, Bernito Mutungile.
Misenyi walioteuliwa ni saba ambao ni Projest Tigamalisho, Florent Kiombo, Asumpta Mshama, Jackiline Rushaygo, Amina Athuman, Nassir Byabato, Pracsud Ndibalema.
“Jimbo la Muleba Kaskazini walioteuliwa ni watano ambao ni Adonis Bitegeko, Charles Mwijage, Fotunatus Muhalila, Dankan Mutagayiwa na Edward Mujungi na Jimbo la Muleba Kusini walioteuliwa ni sita ambao ni Simon Wansulebe, Denis Charles, Dk Oscar Kikoyo, Abdulmajid Ahmada, Dk Modestius Buchard na Dudus Clemence,” amesema.
Jimbo la Ngara walioteuliwa ni Steven Kagaigai, Dotto Bahemu, Harubeti Muhile, Hilary Ruhindwa, Restutha Binambi na Lameck Gaston.