Wakati BDL ikishika kasi mchezo kati ya KIUT na Chui ulilazimika kurudiwa mara tatu baada ya awali kufungana pointi 57-57 katika robo zote nne za mchezo.
Hali ya sare iliendelea pia hata zilipoongezwa dakika tano za nyongeza kwani timu hizo zilifungana 11-11, na kuongezwa dakika tano zingine na kushuhudia sare ya 10-10.
Kutokana na hali hiyo ziliongezwa dakika tano ambazo zilishuhudia Chui ikiibuka na pointi 8-2, jambo lililoifanya Chui iibuke na ushindi wa pointi 88-80, hivyo kufanya mchezo huo uwe pekee ulioongezwa dakika 15 ili kumpata mshindi.
Awali, KIUT iliongoza katika robo ya kwanza kwa pointi 13-6, 19-15 na robo ya tatu na nne Chui ikaongoza kwa pointi 19-13, 17-12.
Mchezaji Louis Victor wa Chui aliongoza kwa kufunga pointi 28, huku Rahim Ramadhan wa KIUT akifunga pointi 26.
Suala la mchezo kuongezwa dakika tano liliendelea kwani mchezo kati ya UDSM Outsiders na Mchenga Stars ulilazimika kurudiwa baada ya timu hizo kufungana pointi 64-64.
Baada ya matokeo hayo ziliongezwa dakika tano za nyongeza ili kupata mshindi ambapo UDSM ilifunga pointi nane na Mchenga ikatupia tatu jambo lililoifanya UDSM iibuke na ushindi wa pointi 72-69.
Katika mchezo huo Marcus Marc wa UDSM alifunga pointi 18 akifuatiwa na Kanyinda Dani aliyefunga 16, huku upande wa Mchenga Stars alikuwa Jamal Hussein aliyefunga pointi 19 akifuatiwa na Peter Chacha pointi 16.
Pointi saba zilizofungwa na Pazi katika muda wa dakika tano za nyongeza katika mechi ya ligi hiyo ziliifanya timu hiyo iishinde ABC kwa pointi 73-71 kwenye mchezo huo uliokuwa wa kusisimua katika Dimba la Donbosco, Upanga.
Katika mchezo huo ABC iliongoza kwa pointi 17-16, 19-19 huku Pazi ikirejea na kutupia 19-19, 11-12 ile ule muda wa nyongeza Pazi ilipata pointi 7-5.