Wanachama 11 wa Chadema waachiwa kwa dhamana Rukwa

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Nyasa, Frank Mwakajoka amesema wanachama 11 wa chama hicho walioshikiliwa na Polisi Mkoa wa Rukwa wameachiwa kwa dhamana.

Mwakajoka amesema pamoja na wanachama hao kuachiwa, Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani na aliyekuwa diwani wa Itete, Albeto Kaliko wote walijisalimisha kwa jeshi hilo na kuachiwa na kesho Alhamisi Julai 31, 2025 wanapaswa kuripoti polisi.

Wanachama hao ni wale ambao Jeshi la Polisi mkoani Rukwa Julai 28, 2025 lilidhibitisha kuwashikilia kwa madai ya kufanya mikusanyiko isiyo halali.

Katika taarifa hiyo ya Polisi, Mbunge wa Nkasi kaskazini, Aida Khenani na Albeto Kaliko aliyekuwa diwani wa Itete walitakiwa kujisalimisha Polisi Wilaya ya Nkasi.

Tofauti na hivyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani hapo kwa kupanga mikusanyiko isiyo halali.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Julai 30, 2025 Mwakajoka amesema; “Jana usiku (Julai 29) wanachama wetu waliachiwa, pia Mbunge wetu na aliyekuwa diwani walijisalimisha na kufanyiwa mahojiano na wameachiwa pia kwa dhamana.”

Mwakajoka amesema wanachama hao pamoja na mbunge wanapaswa kuripoti polisi kwa ajili ya taratibu za mahakamani.

Akizungumzia hatua ya kumshtaki Mkuu wa Kituo cha Polisi Nkasi kama alivyoelekeza Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche amesema utaratibu unaendelea kwa mawakili.

Kwa mujibu wa polisi Julai 28, 2025 waliokamatwa ni wanaume saba wanawake wanne.

Viongozi hao ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana Chadema, Jimbo la Nkasi Kaskazini Winfrida Khenani, Katibu wa Chadema Nkasi Kaskazini, Godfrid Bendera,

Wengine ni Katibu wa Baraza la Wazee Chadema, Evarist Mwanisawa, Mwenyekiti wa Chadema kata ya Majengo, Scolastica Mwalonde,