DAKIKA chache kabla ya mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji Tanzania dhidi ya Burkina Faso uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rayvanny ameibua shangwe kwa mashabiki.
Staa huyo ameingia uwanjani kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo akiimba wimbo wa Kitu Kizito aliomshirikisha Misso Misondo na kuibua vaibu kubwa kwa mashabiki. Baada ya hapo akaimba vionjo vya nyimbo mbili.
Rayvanny hajapata hata dakika moja ya kuimba wimbo mmoja zikapigwa baruti juu ambazo pia zimeibua shangwe na baadae mwanadada Jasinta Makwabe akalipitisha kombe jipya la CHAN.
Pia hajachukua muda kaonyesha kombe hilo kwa mashabiki kisha kutoka nje ya uwanja na taratibu nyingine kuendelea dakika chache kabla ya mchezo kuanza.