Wajumbe Kata ya Kunduchi kuamua leo, Wakili Msomi Happiness Justine Kinyaha yumo

Na Mwandishi Wetu

Wakili Msomi Happiness Justin Kinyaha kupigiwa kura za maoni leo na wajumbe kata ya Kunduchi nafasi ya Udiwani

Wakili Msomi Kinyaha ni mmoja ya wagombea watakao pigiwa kura za maoni na wajumbe leo katika kata ya Kunduchi

Kinyaha ni mmoja ya wagombea watatu ambao majina yake yalirudi baada ya michakato ya vikao vya kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi ya Kata , Wilaya , Mkoa na Halmashauri Kuu kumalizika.

Awali Kunduchi baada vikao walipitisha wagombea watia nia watatu ,baadhi ya wajumbe walitaka kurudishwa wagombea ambapo majina mawili yalirudi na kufanya wagombea kuwa watano kwa Kata hiyo.