Mashahidi kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kufichwa

Dar es Salaam. Mahakama Kuu imeamuru mashahidi wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana) majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kufanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu.

Mahakama hiyo katika uamuzi huo uliotolewa leo Jumatatu Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa, pia imezuia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.

Endelea kufuatilia Mwananchi