Hafla hiyo ilikuwa sehemu ya mashindano ya Vodacom Corporate Masters, yaliyolenga kuhamasisha ushiriki wa wadau kutoka sekta mbalimbali kupitia michezo ya kijamii kama golf.
Tuzo hizo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa kike na wa kiume, wanawake, wanaume pamoja na wachezaji wa golf waliobobea kutoka mashirika tofauti. Kupitia tukio hili, Vodacom iliendeleza dhamira yake ya kuunga mkono michezo, kukuza vipaji na kudumisha uhusiano wa kijamii na wadau wake wa karibu.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Ushirikiano kutoka Vodacom Tanzania Joseph Sayi ( wa pili kushoto) akimkabidhi tuzo moja ya washindi wa tuzo ya gofu ya kupiga mbali Bw. Ali Mamdouhi ( wa pili kulia). Tukio hili limefanyika jana wakati wa ugawaji wa tuzo ulliofanyika na Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam.